Mikopo na sifa za Mkopaji
MKOPO
Utaratibu wa ukopaji: Mikopo yetu hutozwa riba pamoja na bima ya mkopo. Njia inayotumika ni punguzo (Reducing Balance Method).
Utaratibu wa ukopaji: Mikopo yetu hutozwa riba pamoja na bima ya mkopo. Njia inayotumika ni punguzo (Reducing Balance Method).
SIFA ZA MKOPAJI
- Awe amechangia michango kwa muda wa miezi 3 mfululizo.
- Awe mwanachama hai.
- Mkopaji anapaswa kulipa bima ya mkopo kwa ajili ya kinga ya kifo na ulemavu.
- Awe ameweza kurejesha mkopo pamoja na riba yake kulingana na mkataba wake.
- Mkopaji akope mara 3 ya akiba yake.
- Asiwe na mkopo ulioshindwa kulipwa kutoka taasisi nyingine za kifedha.
VIWANGO VYA RIBA
Riba inayotozwa ni 1% kwa mwezi. Mikopo ya dharura, wikendi, na bima hutolewa ndani ya masaa 24 yenye riba ya 5% kwa mwezi kwa baki ya mkopo (Reducing). Viwango hivi vitapungua au kuongezeka kutokana na bei iliyoko sokoni kwa idhini ya mkutano mkuu.
Riba inayotozwa ni 1% kwa mwezi. Mikopo ya dharura, wikendi, na bima hutolewa ndani ya masaa 24 yenye riba ya 5% kwa mwezi kwa baki ya mkopo (Reducing). Viwango hivi vitapungua au kuongezeka kutokana na bei iliyoko sokoni kwa idhini ya mkutano mkuu.
Aina za Mikopo Inayotolewa
Huu ni mkopo ambao mwanachama atakopa kwa kipindi cha mwezi mmoja (1) hadi miezi (36). Mwanachama atajipima kulingana na uwezo wake wa kulipa. Riba ni 1.25% (Reducing balance) kwa mwezi. Ada ya maombi: 1% ya mkopo. Kiwango: TSh 1,600,000 hadi TSh 30,000,000. Mikopo yote ya Maendeleo itaidhinishwa na Kamati ya Mikopo. Hutolewa mwishoni mwa mwezi na fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-15 ya kila mwezi. Bima: TSh 0.8% kwa mwaka.
Unatafuta kujianzisha haraka na kuanza safari yako ya kuelekea uhuru wa kifedha baada ya kujiunga na SACCOS yetu? Mkopo wa Karibu ndilo suluhisho bora kwako. Kama jina lake linavyomaanisha (“Karibu” likiwa na maana ya “welcome”), bidhaa hii imeundwa mahsusi kusaidia wanachama wapya kupata mkopo hata wakiwa na akiba ndogo bila kusubiri kipindi cha kawaida cha miezi 3. Sifa: Upatikanaji baada ya mwezi 1 tu tangu kujiunga. Kiasi: TSh 1,000,000. Muda: miezi 6. Ada: 1%. Riba: 2% kwa mwezi. Hutolewa ndani ya masaa 24. Bima: TSh 0.8% kwa miezi 6.
Suluhisho rahisi kukusaidia kulipia ada za bima. Kiasi: TSh 118,000 – TSh 5,000,000. Muda: miezi 12. Ada: 1%. Riba: 3.5% kwa mwezi (reducing balance). Fedha italipwa moja kwa moja kwa kampuni ya bima. Hutolewa ndani ya masaa 24. Bima: TSh 0.8% kwa mwaka.
Mkopo maalum kwa wanachama waliostaafu. Kiasi kinategemea akiba, hisa, au mafao. Muda: hadi miezi 36. Ada: 1%. Riba: 1.1% kwa mwezi (reducing balance). Dhamana: Hisa au akiba. Hutolewa ndani ya masaa 24. Bima: TSh 0.8% kwa mwaka. Kiasi chini ya TSh 7,000,000.
Huduma ya haraka kwa mahitaji ya dharura. Kiasi: TSh 100,000 – TSh 300,000. Muda: mwezi 1. Riba: 3.4% kwa mwezi. Ada: TSh 3,000. Fedha hutumwa moja kwa moja kwa akaunti ya benki au simu.
Mkopo wa muda mfupi wa miezi sita kwa mwanachama aliyepatwa na dharura. Kiasi: TSh 100,000 – TSh 1,500,000. Riba: 5.5% kwa mwezi. Ada: 1%. Hutolewa ndani ya masaa 24. Bima: TSh 0.8% kwa miezi 6.
Mkopo maalum kwa gharama za elimu. Kiasi: TSh 500,000 – TSh 5,000,000. Muda: miezi 12. Riba: 1% kwa mwezi. Ada: 1%. Malipo yatafanyika moja kwa moja kwa akaunti ya shule au chuo. Bima: TSh 0.8% kwa mwaka.
Mkopo wa muda mfupi wa mwezi 1 hadi 2. Kiasi: TSh 50,000 – TSh 500,000. Riba: 3.5% (Reducing balance). Ada: TSh 3,000. Hutolewa ndani ya masaa 24. Bima: TSh 0.8% kwa miezi 2.
Mkopo wa muda wa mwezi 1 hadi 24. Riba: 1.35% (Reducing balance). Ada: 1%. Kiwango: TSh 1,600,000 – TSh 10,000,000. Hutolewa baada ya tathmini ya biashara. Mwanachama atakopa mara 3 ya akiba zake.
Kumbuka: Wanachama haruhusiwi kuchukua mkopo wa aina moja zaidi ya mara moja. Pia mwanachama anaweza kutopopewa mkopo hadi akatwe asilimia 50% ya mkopo.
Jedwali Na.1: Viwango vya Mikopo na Riba, Muda na Kinga ya Mkopo
| Aina ya Mkopo | Kiasi cha Mkopo (TSh) | Ada (%) | Riba (%) kwa Mwezi | Muda (Miezi) | Kinga (%) | Adhabu (%) kwa rejesho lililochelewa |
|---|---|---|---|---|---|---|
| Maendeleo | 30,000,000 | 1 | 1.25 | 36 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Elimu | 5,000,000 | 1 | 1 | 12 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Dharura | 1,500,000 | 1 | 5.5 | 6 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Wikendi | 500,000 | 3,000 (fixed) | 3.5 | 2 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Bima Advance | 5,000,000 | 1 | 3.5 | 6 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Karibu | 1,000,000 | 1 | 2 | 6 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Wastaafu | 7,000,000 | 1 | 1.1 | 36 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Papo Hapo | 300,000 | 3,000 (fixed) | 3.4 | 1 | 0.8 | 10 kwa mwezi |
| Biashara | 10,000,000 | 1 | 1.4 | 24 | 0.8 | 10 kwa mwezi |